Simba wawapagawisha Wabunge

Dimba - - Dimba Special - NA RAMADHAN HASSAN,DODOMA

KAMA ni mapenzi basi wanayo Wabunge mashabiki wa Simba kwani mara baada ya timu hiyo kutinga bungeni hali ya hewa ilibadilika mara baada ya Mwenyekiti wa Bunge,Najma Giga kuitambulisha timu hiyo.

Wakati akitaka kuuliza swali Mbunge wa Ilala,Musa Zungu (CCM) alipiga vijembe kwa kusema kudai kwamba humu ndani ameingia mnyama mkali lakini tupo salama hali iliyoibua shangwe kubwa na makofi.

Simba ilifanya ziara maalumu Bungeni kwa ajili ya kupongezwa na wabunge mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakifurahia timu hiyo kutwaa ubingwa mara baada ya kupita misimu minne bila taji.

"Humu ndani ameingia mnyama mkali lakini tupo salama," alisema Najma.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.