Chuoni yasalia Ligi Zanzibar

Dimba - - Dimba Special - NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR

KLABU ya Chuoni imejihakikishia kubaki Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya kuifunga mabao 2-0 KMKM katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Zanzibar Kanda ya Unguja. Mabao ya Chuoni yamefungwa na Hamadi Mshamata dakika ya 10 ya mchezo kipindi cha kwanza na lile la dakika ya 70 baada ya kuunganisha mpira uliotoka kwa winga Salum Kimuungoni. Akizugumza na DIMBA Jumatano, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Suleiman Jabir, alipongeza wachezaji wake kwa ushindi walioupata na kuwataka kukaza buti.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.