Bocco akwepa mtego wa mashabiki Simba

Dimba - - Dimba Special - NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

HII kali. Mashabiki wa soka wa Mtaa wa Gwassa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma Combine, walikuja na gari kwa ajili ya kumchukua straika wa timu hiyo, John Bocco. Eti walidai kwamba Bocco ndio kila kitu hivyo wanataka kumpeleka geto ili akawaone mashabiki wa timu hiyo jinsi wanavyompenda. Juma Matokeo alisema: “Bocco ndio kila kitu usafiri upo pale nje gemu ikiisha tu tunasepa naye ili washkaji walio home wakamuone.” Mara baada ya kumalizika kwa mtanange huo, mashabiki hao walimfuata mshambuliaji huyo lakini alikimbilia kwenye basi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.