Simba ifanye nini ili kufika mbali kimataifa?

S IMBA imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, hivyo ndiyo itakuwa mwakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Dimba - - Dimba Special - DAR ES SALAAM

Kwa takribani miaka mitano, Simba haijaweza kutwaa ubingwa, hivyo kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa, ingawa msimu wa mwaka jana iliweza kutwaa taji la Kombe la Shirikisho na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu. Lakini hata hivyo, walishindwa kufika mbali kwenye mashindano hayo kutokana na kutoshiriki kwa muda mrefu na kushindwa kujipanga vema na kuishia kwanye hatua ya kwanza, baada ya kutolewa na Al Masry ya nchini Misri. Sasa wanakwenda rasmi Klabu Bingwa Afrika baada ya kuibuka kuwa mabingwa msimu huu, ukiwa kama mdau wa soka nchini unaishauri nini timu hiyo? Wanahitaji kufanya nini ili kufanya vema msimu ujao kwenye michuano ya kimataifa na wasiwe kama ilivyofanya mwaka huu? Tuma maoni yako, ukianzia na jina lako kamili na mahali ulipo kwenda namba 0718540757. WIKI iliyopita kulikuwa na mada inayozungumzia juu ya mwenendo mbaya wa Yanga kwa sasa kwenye mechi zake za Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, je, timu hiyo ilikosea wapi? Yanga imekuwa haina matokeo mazuri kwa sasa na tangu kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu George Lwandamina, haijashinda hata mchezo mmoja wa Ligi wala michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Lakini pia suala la kuyumba kiuchumi limezidi kuiumiza klabu hiyo na kusababisha baadhi ya wachezaji kugomea kucheza baadhi ya mechi. Wachangiaji wengi walituma maoni yao juu ya suala hilo na wengi wakiamini kuwa ukata, majeruhi na usajili ndivyo vilivyoiumiza zaidi timu hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.