Iniesta bado pasua kichwa

BAADA ya kutangaza kuwa hatakuwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania, Barcelona, kiungo Andres Iniesta amesema kuwa, bado hajajua anakwenda wapi hadi sasa, kama ni China au Japan.

Dimba - - Dimba Special -

Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, bado yupo njiapanda ya kwenda China, Japan au Australia, bado hajathibitisha anakwenda wapi.

Iniesta, mwenye umri wa miaka 34, anaondoka Barca akiwa ameisaidia kutwaa taji la La Liga, huku akiwa amedumu katika timu hiyo kwa miaka 16.

"Nitafanya maamuzi ambayo yatakuwa muhimu kwangu.

"Wiki ijayo naamini nitatoa jibu sahihi. Lakini hivi sasa akili yangu ipo katika fainali za kombe la Dunia,” alisema hayo, alipokuwa akihojiwa na kituo cha Onda Cero.

Kiungo huyo hadi sasa amecheza michezo 43 katika mashindano yote, huku akikisaidia kikosi cha Barca kushinda La Liga pamoja na Copa del Rey.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.