MANCINI AMREJESHA BALOTELLI KIKOSINI

Dimba - - Dimba Special - MILAN, ITALIA

KOCHA Roberto Mancini ambaye atakuwa na timu ya Taifa ya Italia, amesema milango iko wazi kwa Mario Balotelli kurejea kikosini.

Mancini aliyasema hayo katika mahojiano yake ya kwanza na waandishi wa habari baada ya kutajwa kuwa ndiye atakayeiongoza Italia iliyoshindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Baada ya kupewa kibarua hicho, gumzo kubwa lilikuwa ni hatima ya Balotoelli kwa kuwa alikaribia kuzichapa na Mancini wakati walipokuwa Manchester City.

"…Italia inahitaji wachezaji wa kiwango cha juu. Nitazungumza na Balotelli," alisema Mancini na kuongeza: "Umri ni muhimu kwa sababu tunataka kuwa na kesho yetu," alisema Mancini.

Baada ya kushindwa kung’ara England akiwa na Liverpool, Balotelli mwenye umri wa miaka 27, amekuwa hatari akiwa Nice, ambako amepachika mabao 43 kwa misimu yake miwili Ligi Kuu Ufaransa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.