KOCHA SIMBA AVUNJA MAZOEZI KISA YANGA

Dimba - - Front Page - NA MWANDISHI WETU

SIMBA leo jioni ilikuwa wafanye mazoezi yao ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar, lakini Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Pierre Lechantre, ameamua kusitisha programu hiyo ili kwenda kuishuhudia Yanga ikicheza na Rayon Sports.

Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, leo kuanzia saa 1:00 usiku watakuwa wenyeji wa Rayon Sports ya Rwanda, ikiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa USM Alger ya Algeria.

Kutokana na hali hiyo, kocha huyo wa Simba amewaambia vijana wake badala ya kufanya mazoezi jioni, wanatakiwa kufanya asubuhi ili usiku wapate nafasi ya kwenda Uwanja wa Taifa, kushuhudia kipute hicho kati ya Yanga na Rayon.

Pierre ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, wanatamani kuona mchezo huo wa watani zao wa jadi ndiyo maana ameshauri mazoezi yafanyike asubuhi badala ya jioni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.