Yanga yamwondoa Kabwili Ngorongoro

Dimba - - News - NA MARTIN MAZUGWA

TIMU ya Yanga imemrudisha kikosini mlinda mlango wake chipukizi, Ramadhan Kabwili, ambaye alikuwa katika kambi ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, ambayo ipo katika maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Mali.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Meneja wa kikosi hicho, Hafidh Saleh, alisema kuwa, wameamua kumrudisha Kabwili ili kumsaidia kipa namba moja, Youthe Rostand, katika mchezo huo watakapowakabili Rayon Sport katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho, utakaopigwa kesho, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga wamechukua hatua ya kumrudisha kikosini Kabwili kutokana na uhaba wa walinda mlango, baada ya Beno Kakolanya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, uliopigwa jijini Mbeya.

“Tumemrudisha Kabwili ili kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi, hasa kipa, kwa sababu tulikuwa na kipa mmoja tu, Rostand, hivyo kumwongeza Kabwili ni sehemu ya mikakati ya kuifanya timu kuwa imara,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.