Darts wapongezwa uteuzi timu ya Taifa

Dimba - - News - NA VALERY KIYUNGU

WADAU wa mchezo wa darts, maarufu kama vishale wa maeneo mbalimbali nchini, wamepongeza uteuzi wa timu ya taifa ya Chama cha Darts cha Tanzania (Tada) na kusema kuwa, inaweza kuleta ushindi katika mashindano ya kimataifa.

Hivi karibuni Tada kilitangaza kikosi cha majina ya wachezaji 12, wakiwamo wanawake wanne, ambacho kitashiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki, yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika Jiji la Nairobi, nchini Kenya.

Wakizungumza na DIMBA kwa nyakati tofauti, wadau hao wakiongozwa na Eliuteri Mtenga, walisema uteuzi wa timu hiyo umezingatia weledi, nidhamu na uwezo wa wachezaji, hivyo wanaamini itaweza kufanya vizuri kimataifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.