Tanzania mwenyeji FIBA Zone Five U-18

Dimba - - News - NA SHARIFA MMASI

UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), umetoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kuboresha Uwanja wa Ndani wa Taifa, utakaotumika kufanikisha michuano ya Kanda ya Tano (FIBA Zone 5) kwa vijana wenye miaka chini ya 18.

Michuano hiyo, ambayo itashirikisha nchi mbalimbali za Afrika, imepangwa kuanza Juni 17-22, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Rais wa TBF, Phares Magesa, alisema mashabiki wa mpira wa kikapu wamekuwa wakiulalamikia Uwanja wa Ndani kuwa hauna ubora, hivyo anaomba Serikali na wadau mbalimbali waone umuhimu wa kuufanyia ukarabati.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.