Thea bado hajaona mpinzani Bongo Movie

Dimba - - Burudani za wasani - NA JESSCA NANGAWE

MKONGWE wa filamu hapa nchini, Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea, amesema mpaka sasa hakuna staa mpya wa kike anayemsumbua kwenye tasnia hiyo hivyo wakaze buti ili waweze kuendana na ubora wake.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Thea alisema bado anatengeneza kazi nzuri ambazo zimekuwa zikimwongezea mashabiki na kumpa moyo wa kuendelea kufanya kazi nzuri kila kukicha.

“Bado hakuna staa mpya anayeweza kunifikia, nimekaa kwenye sanaa ya filamu kwa zaidi ya miaka 20 na tayari nimetengeneza filamu zaidi ya 50, najivunia uwezo wangu na ndio maana watu hawachoki kunitazama,” alisema Thea.

Alisema, anachoshauri kwa wasanii wanaochipukia kwenye tasnia hiyo ni kujituma kwa umakini kuhakikisha hawaridhiki na kile kidogo wanachokipata.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.