Wolper: Sina muda wa kulumbana na Harmonize

S TAA wa filamu nchini, Jackline Wolper, amesema hana muda wa kulumbana na mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Harmonize na badala yake anawaza namna ya kutunisha akaunti yake kifedha.

Dimba - - Burudani za wasani - NA JESSCA NANGAWE

Wolper na Harmonize wamekuwa wakitupiana vijembe kupitia mitandao ya kijamii, hali ambayo imezusha sintofahamu kupitia kwa mashabiki zao. Wolper amesema kikubwa kwa sasa habari mbaya zinazozungumzwa juu yake anamwachia Mungu na anachoangalia kwa sasa ni jinsi ya kuingiza fedha na si kutengeneza habari kupitia jina lake. “Unajua wengi wanatamani nimjibu Harmonize, lakini watambue Wolper wa sasa hivi si yule wa miaka ya zamani, najaribu kujiheshimu na kuendana na hali ya maisha si kutumia muda wangu kuzozana kwenye mitandao,” alisema Wolper.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.