Aunty Ezekiel aota tuzo filamu ya 'Mama'

Dimba - - Burudani za wasani - NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kuzindua filamu yake ya 'Mama' mapema mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Mlimani City, staa wa filamu nchini, Aunty Ezekiel, amejinasibu kuwa kazi hiyo itampatia tuzo za kutosha kutokana na ubora wake.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Aunty alisema ubunifu aliotumia kukamilisha filamu hiyo ni wa hali ya juu na anaamini mapokezi yake yatakuwa makubwa tofauti na kazi zake za awali.

“Nilitumia muda mwingi na fedha kuhakikisha hii filamu inakuwa ya kuigwa, naamini kabisa itanitambulisha zaidi, nategemea hata tuzo nyingi zaidi nitazipata ila nawashukuru wote ambao wametumia muda wao mwingi kunisapoti katika hili,” alisema Aunty.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.