UKUTA WA YANGA UMEPATA UFA

Dimba - - Dimba Special -

ACHANA na timu ya Yanga kucheza jumla ya michezo saba bila kuibuka na ushindi mashindano yote tangu kuondoka kwa kocha wao mkuu, George Lwandamina, kubwa jingine ni kikosi kilivyoruhusu mabao mengi zaidi wakiwa bado na michezo minne mkononi. Kikosi hicho kilichopo chini ya kocha Mcongo, Zahera Mwinyi ambaye hajakamilishiwa mambo kadhaa na uongozi kusimama katika benchi, hadi sasa kimeruhusu wavu wake kuguswa mara 17 tofauti na msimu mzima uliopita, kwani kilifungwa mabao 14 pekee. Licha ya kubadilisha makipa wote watatu, Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili na kusimama langoni hapo mara kadhaa kwa nyakati tofauti, lakini bado wameshindwa na mlinda mlango mmoja pekee, Aishi Manula wa Simba aliyefungwa mabao 13.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.