UMEWASOMA KAPOMBE, CHILUNDA, PETER

Dimba - - Dimba Special -

ALIANZA Idd Shabani ‘Chilunda’ mwishoni mwa wiki kuifungia timu yake ya Azam katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji, kabla ya siku moja baadaye Shomari Kapombe kumtungua Ally Msitapha ‘Barthez’ michezo yote ya Ligi Kuu Bara. Lakini pia Jumapili, Paul Peter akifunga bao pekee la kufutia machozi katika kichapo walichokutana nacho timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes dhidi ya Mali. Wakati Kapombe akifunga bao lake hilo la kwanza tangu atue Simba msimu huu akitokea Azam, lakini pia ilikuwa wikiendi tamu kwa matajiri hao wa Bongo kuwashuhudia vijana wao Chilunda na Peter wakitimiza majukumu yao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.