NYOTA YAKO WIKI HII

Mnajimu Ramadhani Yahya atakuwepo Dar kwa mwezi mmoja kabla ya ziara nyingine ya Dubai, anapatikana Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam au Hale mkoani Tanga, simu namba 0652 545462, Instgram Mnajimu Mkuu.

Dimba - - Dimba Special -

NG'OMBE (TAURUS) (April 21-Mei 21)

Utakabiliwa na ishara ya ndoto mbaya na zinazohusu familia na maisha kwa jumla, hii ni dalili nzuri ya kuvuka vikwazo vilivyokuwa vinakukabili, hii ni wiki njema kwa kuomba dua na kupata tija.

MAPACHA (GEMINE) (Mei 22- Juni 21)

Kabla hujaamua kufanya tukio kubwa litakalokukabili wiki hii, ni vizuri kupata ushauri wa kinyota, utapata maombi ya kifamilia ni vizuri kuyathamini.

KAA (CANCER) (Juni 22-Julai 23)

Malalamiko yaliyokuwa yakikukabili toka sehemu zako za kupata riziki yataisha katika hali njema, unatakiwa kuanzisha mipango mipya ili kupata mahitaji yako, acha kuendelea na yale yale yaliyopita.

SIMBA (LEO) (Julai 24-Agosti 23)

Bahati ya kipato itakuwepo wiki hii, matatizo madogo sasa yatapungua, ni kipindi kizuri kwa kuanzisha jambo jipya maana litapata mafanikio makubwa kwa wenye nyota hii.

MASHUKE

(VIRGO) (Agosti 24-Septemba 23)

Juhudi zako zitaanza kuzaa matunda tena baada ya kusimama, mambo yako ya maendeleo pia yatafunguka na kukuondoa hapo ulipo, tumia muda wako mwingi kutengeneza maisha yako ya baadaye.

MIZANI (LIBRA) (Septemba 24-Oktoba 23)

Unalofikiria litakusaidia linaweza kuwa mzigo kwako, jiepushe kuingia katika urafiki uliojaa dharau na kuchunguzana yapo mambo mengi yanapotea kwa ajili ya kukatishwa tamaa.

NGE (SCROPION) (Oktoba 24-Novemba 22)

Unaweza kulazimika kutoa msaada kwa ajili ya mgonjwa au sherehe, hizi ni alama za kukumbusha juu ya ahadi ulizoahidi na kisha kuacha kuzitekeleza, ni vuzuri kutoa sadaka ili lkuvuta bahati wiki hii.

MSHALE (SAGITARIUS) (Novemba 23-Desemba 21)

Una siku mbili unazotakiwa kuchagua kutimiza ahadi ya mahusiano uliyoipanga wiki hii, utapata shida ya kupata usingizi usiku na pia hali ya kuogopa bila sababu ni dalili za kufanyiwa uadui.

MBUZI (CAPRICON) (Desemba 22-Januari 20)

Hiki ni kipindi cha neema kwako, utakaa mbali na dhiki kama maradhi na hata mawazo ya moyoni yatapungua, endapo kama bado utakuwa ukiandamwa na shida na mikosi basi amini lipo jambo la ziada usisite kutafuta ushauri.

NDOO (AQUARIUS) (Januari 21-Februari 19)

Unajilazimisha jambo fulani ili umridhishe mtu, mwenyewe unatambua hili, kinyota hizo si njia nzuri zitakazokuvusha katika malengo yako, unashauriwa kufanya mambo yako wewe mwenyewe ya binafsi ndiyo yenye tija wiki hii.

SAMAKI (PISCES) (Februari 20-Machi 20)

Matarajio uliyokuwa nayo ya kupata jambo fulani, yatayeyuka hii ni kutokana na kuanadamwa na mikosi, unachotakiwa kufanya ni kurudi katika maombi kabla ya kulala na kuwahi kuamka ili kuzikwepa hujuma za usoni mwa binadamu.

PUNDA MACHI (Machi 21-April 20)

Wazo lako la kutaka kubadilisha aina ya maisha litafanikiwa na wenye safari za kikazi au kibiashara zitakuwa na tija kwao, hata hivyo wanatakiwa kupanga mambo yao mengi usiku na kwa njia ya kificho ili kuepuka hujuma zinazoiandama nyota hii.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.