Kazi ya lawama

M OJA kati ya kazi ngumu zaidi duniani ni hii ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil. Unaweza kujikuta unameza Panadol kila siku kabla ya kwenda kazini.

Dimba - - Dimba Special - kuonekana na kupata nafasi ya kucheza Brazil miaka ijayo.

ichuano hiyo mikubwa duniani. Nyota hao ni Alisson, Cássio, Ederson; Danilo,... Kuelekea Kombe la Dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Russia, kocha wa Brazil, Tite, amejilipua na kuita kikosi cha wachezaji 23 tu watakaoliwakilisha taifa hilo katika michuano hiyo...

Inaaminika kila raia wa Brazil ana kipaji cha kucheza soka. Iwe fundi baiskeli au dereva wa daladala. Sasa mtihani huja pale kocha unapotakiwa kuita kikosi cha wachezaji 23 tu. Utamwita nani utamwacha nani? Full lawama! Kuelekea Kombe la Dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Russia, kocha wa Brazil, Tite, amejilipua na kuita kikosi cha wachezaji 23 tu watakaoliwakilisha taifa hilo katika michuano hiyo mikubwa duniani. Nyota hao ni Alisson, Cássio, Ederson; Danilo, Geromel, Filipe Luís, Marcelo, Marquinhos, Miranda, Fagner, Thiago Silva; Casemiro, Fernandinho, Fred, Paulinho, Coutinho, Renato Augusto, Willian, Douglas Costa, Firmino, Gabriel Jesus, Neymar na Taison. Si umeona mziki ulivyoshona huo? Sasa unaambiwa tayari Tite ameshashushiwa zigo la lawama kwa madai kuna wachezaji wengine watano ambao watu wanaona walistahili kuwemo kwenye kikosi hicho.

Alex Sandro

Alex Sandro hakuwa kwenye kiwango bora kipindi hiki kulinganisha na alivyokuwa msimu wa 2016/17, lakini bado ni miongoni mwa mabeki bora wa kushoto barani Ulaya. Bahati mbaya kwake Marcelo na Filipe Luis wako vizuri zaidi yake. Tangu mwaka 2011, Sandro amecheza michezo 100 akiwa na kikosi cha Brazil na hivi karibuni aliitwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Russia, lakini kumbe ilikuwa ni kwa sababu Filipe Luis alikuwa majeruhi.

David Luiz

Kuna beki mwenye uchungu na jezi ya Brazil kama David Luiz? Mara zote anapopangwa hucheza kwa uwezo wake wote. Bahati mbaya kwake hakuwa na msimu mzuri msimu huu katika klabu ya Chelsea kiasi cha kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza. Majeraha pia yanatajwa kuwa sababu ya msingi iliyomfanya Luiz kuwa nje ya mipango ya kocha wa ‘The Blues’, Antonio Conte. Huenda hii ilikuwa nafasi yake ya mwisho kucheza Kombe la Dunia lakini imeshindikana. Pole sana Luiz.

Fabinho

Hata Fabinho? Nani alitegemea kama Tite angempiga chini nyota huyu. Baada ya Dani Alves kuumia, wengi walikuwa wakimpa nafasi ya kwenda Russia, lakini mambo yamekuwa kinyume. Hajaitwa kabisa kikosini. Beki huku wa kulia wa klabu ya AS Monaco, ana uwezo pia wa kucheza kwenye nafasi ya kiungo, amekuwa katika kiwango bora msimu huu na iliaminika angekuwa msaada kwa Tite. Nafasi yake wameitwa Fagner na Danilo. Uamuzi uliolalamikiwa na mashabiki wengi wa Brazil. Unajua kwanini? Fagner ndio kwanza anarejea baada ya kupona jeraha lake la nyama za paja huku Danilo akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Man City msimu huu.

Talisca

Jina lake kamili ni Anderson Souza Conceição, lakini mwenyewe hupenda kuitwa Talisca. Huyu ni miongoni mwa viungo bora barani Ulaya msimu huu.

Akiwa na Besiktas msimu huu amefunga mabao 19 na kutoa asisti 5. Yuko kwenye kiwango bora sana lakini kwa Tite jicho lake lilikwenda kwa Philippe Coutinho, Willian, Taison na Douglas Costa.

Kwa wanne hao, Talisca anaweza kulalamika kuwa ni bora zaidi ya Taison tu. Hao waliobaki yeye itakuwa dhambi akisema lolote.

Kwa sasa anachoweza kufanya ni kutoka Besiktas na kusaka timu kubwa zaidi barani Ulaya ili iwe rahisi kwake

Felipe Anderson

Huyu jamaa hana bahati aisee. Fundi huyu wa Lazio yuko kwenye kiwango bora msimu huu, lakini imekuwa majanga kwake kwani Renato Augusto na Paulinho wako njema zaidi.

Lakini pia Felipe ana uwezo wa kucheza kama winga wa pembeni lakini si kweli kama Tite angefikiria kumwita na kuwaacha Willian na Douglas Costa.

Pale mbele ndio kabisa hapamfai. Roberto Firmino na Gabriel Jesus wako moto balaa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.