Yanga mikononi mwa Kamusoko

KUNA kila dalili ya Yanga kuikosa huduma ya kiungo wao mahiri, Papy Kabamba Tshshimbi, ikielezwa amerejea nyumbani kwao, Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kujitibu majeraha yake ya goti.

Dimba - - Dimba Special - NA MAREGES NYAMAKA

kupoteza pointi zote sita kwenye mechi hizo. Kucheza kwake tayari atakuwa amepata utimamu wa mwili kuiongoza Yanga ambayo inapitia wakati mgumu kuingia eneo la ulinzi na safu ya ushambuliaji inatorajiwa kuongozwa na kinara wao wa mabao, Obrey Chirwa. Umahiri wake wa umiliki

Nyota huyo tangu alipoumia moja ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kabla ya kujitonesha dhidi ya Simba, ubora wake unajulikana kwa kila mdau wa soka Tanzania namna timu ilivyokuwa ikitembea mgongoni kwake hasa eneo la kiungo alivyoiunganisha.

Bahati mbaya wakati anawasili mkali huyo wa zamani wa klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland, hakufaidi muunganiko wake na Thaban Kamusoko kutokana na Mzimbabwe huyo kukumbwa na majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kurejea kwa Kamusoka hivi karibuni tayari akiwa na mechi mbili ngumu hadi sasa dhidi ya timu za Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar, kwa nyakati tofauti akipishana na Tshishimbi, hiyo inamfanya itembee mabegani kwake.

Katika mechi hizo ambazo zilikuwa ni miongoni mwa maandalizi ya mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho (Caf) dhidi ya Rayon Sport Rwanda. Tayari Kamusoko alionyesha kurejea kwenye kiwango chake kiasi kikubwa achilia mbali mkubwa wa mpira akiwa na wastani mzuri wa kutengeneza nafasi, nyuma yake kuna Said Juma ‘Makapu’ atakuwa anatimiza jukumu lake la kwanza la kuwalinda mabeki wake kuhakikisha kwamba lango lake halishambuliwi. Tunatambua hapo kabla ya Yanga kuyumba hasa msimu huu, katika michezo sita iliyopita baada ya kuondokewa na kocha wao mkuu, George Lwandamina, uti wa mgongo wa kikosi hicho mbali na Tshimbishimbi wapo Kelvin Yondani na Obrey Chirwa. Wawili hawa ambao walikosekana mechi mbili zilizopita kutokana na sababu tofauti, uwapo wa Kamusoko sambamba na mbinu kutoka benchi la ufundi naiona nafasi kubwa ya Yanga kushambulia zaidi kwa kutumia pasi fupifupi na ndefu pale inapopaswa kufanya hivyo. Jambo nzuri ni kwamba, Yanga wanakutana na kikosi ambacho pia kinaonekana kusuasua kwenye ligi yao (Rwanda National Football League), kikicheza michezo zaidi ya mitano bila kupata ushindi na kuwafanya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi zao 36. Lakini hiyo haitoi taswira kuwa ni wa kawaida wanaweza kufungika kirahisi la hasha, linapokuja suala a michuano tofauti ambayo ni ya mtoano, mipango ya kocha inakuwa taofauti kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza walipowalazimisha Gor Mahia ya Kenya sare ya bao 1-1.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.