Warriors yaichapa Rockets vikapu 119-106

LICHA ya kufanya vizuri kwa kufunga pointi 41 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya NBA, James Harden hakuisaidia timu yake ya Houston Rockets kuepuka kichapo cha vikapu 119-106 mbele Golden State Warriors, waliokuwa nyumbani.

Dimba - - Dimba Special -

Mchezo huo wa Kanda ya Magharibi ulipigwa katika Uwanja wa Oracle Arena, huko California, umewapa uongozi wa 1-0 Golden State katika mtanange wa kwanza wa nusu fainali.

Mtanange huo uliokuwa na upinzani mkubwa mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa kila moja ikiwa na vikapu 56. Mambo yalibadirika raundi ya tatu baada ya State kuongoza kwa pointi 13 na kuwafanya Rockets kupoteza tumaini.

Nyota aliyekuwa mwiba kwa Rockets alikuwa Kevin Durant, ambaye alifunga vikapu 37, huku nyota aliyemfuatia akiwa Klay Thompson, ambaye alifunga vikapu 28.

Naye mlinzi wa Houston, Chris Paul, ambaye huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza wa nusu fainali ya NBA tangu alipoanza kucheza kikapu, alifunga vikapu 23, huku mipira iliyorudi ‘rebounds’ ikiwa 11.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.