DE BRUYNE: MAN CITY HAIKAMATIKI TENA

K EVIN De Bruyne amesema itakuwa ngumu kwa wapinzani wao Ligi Kuu England kuweza kuifikia rekodi waliyoiweka msimu huu ya kumaliza mbio za ubingwa wakiwa na pointi 100.

Dimba - - Dimba Special -

Kwa idadi hiyo, Man City waliweza kuipiku Chelsea ambayo ilikuwa ikishikilia rekodi hiyo walipochukua ubingwa kwa pointi 95.

"Tulijua kabisa kuwa tukifikisha pointi 100, litakuwa jambo la kipekee na itakuwa ngumu kwa wengine kutufikia," alisema De Bruyne.

Naye nahodha wa kikosi hicho ambaye msimu huu amechukua ubingwa wake wa tatu akiwa Etihad, Vincent Kompany, alisema Pep Guardiola ndiye kocha bora ulimwenguni.

"Hakuna ubishi, naaminin ni kocha bora na anawajua wachezaji wazuri, amefanya makubwa," alisema Kompany.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.