KICHUYA, OKWI WATOA YA MOYONI

Dimba - - News - SAADA SALIM NA CLARA ALPHONCE

BAADA ya kulazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya Yanga mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumapili ya wiki iliyopita, baadhi ya wachezaji wa Simba, wametoa ya moyoni wakionyesha kuumizwa na matokeo hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachezaji hao walisema kwa jinsi walivyokuwa wamejipanga ilikuwa lazima Yanga wafungwe, lakini dakika 90 zikamalizika timu hizo zikitoshana nguvu kwa suluhu hiyo ya 0-0.

Winga machachari wa kikosi hicho, ambaye mara kadhaa amekuwa na bahati ya kuwafunga Yanga, Shiza Kichuya, alisema kila mmoja aliyekuwa akiangalia mpira ule aliona jinsi walivyopambana kuhakikishia wanapata ushindi, lakini hajui kilichotokea mpaka matokeo yakawa suluhu.

“Mimi nadhani hata mashabiki wengi na hata wasiokuwa upande wetu waliona namna tulivyojituma, tulijipanga sana ili kuwapa furaha mashabiki wetu, lakini mambo yakaenda kinyume, kwani tulitoka sare, yani hata sisi wachezaji hatukuamini zilipomalizika dakika 90,” alisema.

Kwa upande wake Emmanuel Okwi, alisema bahati haikuwa upande wao, kwani walitengeneza nafasi nyingi, lakini mipira ikashindwa kutumbukia kambani, ila sasa wanaelekeza nguvu zao michezo inayokuja.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.