Faru Dume, Malamba FC zatakata Ubungo

Dimba - - News - NA VALERY KIYUNGU

TIMU ya Faru Dume ya Manzese na Juhudi FC ya Mabibo, juzi zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika mechi ya Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Ubungo, iliyopigwa Uwanja wa Kinesi, jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Juhudi FC yalifungwa na Abdul Omary na Sharifu Yahaya wakati yale ya Faru Dume ‘Muso’ yaliwekwa wavuni na Nyai Shida na Abdallah Makuburi.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo timu ya Malamba FC iliichapa AS Kibamba mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ukombozi, Manzese.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.