Gidabuday achekelea wanariadha Majeshi

Dimba - - News -

NA GLORY MLAY KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhem Gidabuday, amesema nyota ya riadha hapa nchini itaanza kuchanua tena baada ya wanariadha waliopo jeshini kuruhusiwa kushiriki michuano ya kimataifa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Gidabuday alisema wanariadha wengi ambao wanaliletea sifa taifa mara nyingi wamekuwa wakizuiwa jeshini kutokana na kubanwa na majukumu ya mwajiri wao.

“Sasa riadha Tanzania itaanza kung’aa kwani wanariadha wetu ambao walikuwa wakishndwa kushiriki mashindano mbalimbali sasa wataanza kupewa nafasi za kusaka medali kimataifa ili tuirudishe heshima yetu kimataifa,” alisema.

Alisema wanariadha wachache wamekuwa wakishiriki mashindano ya kimataifa na kufanya mchezo huo kupoteza ladha, lakini sasa tumaini limerudi upya na wanaamini medali zitavunjwa nyingi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.