Queen Darleen kwa mapenzi ya siri hajambo!

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongo Fleva, Mwanahawa Abdul maarufu ‘Queen Darleen’, amesema haiwezi kutokea kwake kufanya uamuzi kumwanika mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa haoni sababu ya kufanya hivyo.

Msanii huyo wa kike pekee kutoka lebo ya WCB, amefunguka kuwa moja ya mambo anayoyaamini ni kutunza mapenzi yake kwa yule anayempenda hivyo haitatokea kwa yeye kumwanika hadharani.

“Ni ngumu kumweka mpenzi wangu kwenye mitandao, mambo ya uzushi kwangu siyapi nafasi na ninachoangalia ni kulinda jina langu, watambue mimi ni mtoto wa kike na ninajua thamani ya mwanaume wangu hivyo ni ngumu kumwanika,” alisema mrembo huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.