Sanchez katika kiza kinene Man United

Dimba - - Mbele - MANCHESTER, England

HIVI ile jezi namba 7 ya Manchester United ina nini? Nafikiri hilo ni swali ambalo utakuwa unajiuliza kuhusu namba hiyo yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo maarufu duniani. Historia yake inaonyesha wachezaji waliovaa jezi hiyo walikuwa na uwezo mkubwa na kuandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu zisizofutika ndani ya Old Trafford. George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo, ni majina ya wachezaji waliokuwa na historia kubwa walipovaa jezi hiyo nzito pale Manchester United. Baada ya kuitwa Ligi Kuu England mwaka 1992, Cantona alitinga jezi hiyo akitokea Leeds United na kufanikiwa kucheza michezo 156, alifunga mabao 70 na kutoa asisti 56 katika misimu mitano aliyokuwa Manchester United. Kuondoka kwa staa huyo wa Ufaransa milango ilifunguliwa kwa kijana aliyetoka katika akademi ya timu hiyo, Beckham, ambaye aliitumikia Manchester United kwa misimu 11. Beckham alitambulika kama mfalme wa mipira iliyokufa lakini alijitambulisha katika ulimwengu wa soka kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga krosi zilizozua balaa kwa wapinzani. Katika misimu hiyo 11 aliyokuwa na Red Devils, alifanikiwa kucheza michezo 265, alifunga mabao 62 na kutoa asisti 80. Historia iliendelea kuandikwa baada ya Manchester United kumsajili Ronaldo kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, huku ikielezwa kuwa

kijana huyo aliyekuwa na miaka 18 alihitaji kuvaa jezi namba 28. Lakini kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliamini uwezo wa kijana huyo si wa kuvaa jezi hiyo aliyoitaka bali namba 7 ilikuwa bora zaidi kwake. Tangu hilo kutokea iliandikwa historia kubwa ndani ya Old Trafford kwa Ronaldo kufunga mabao 84 na kutoa asisti 34 katika michezo 196 ya Ligi Kuu England kwa misimu sita kabla ya kutimkia Real Madrid na sasa Juventus. Licha ya kuwataja hao katika mafanikio ya jezi hiyo yenye historia kubwa Manchester United, alikuwepo Best ambaye inaamika ndiye mchezaji bora kuwahi kuvaa namba 7 ndani ya Old Trafford. Best alikuwa mmoja wa wachezaji waliotengeneza utatu mtakatifu mkali wa kikosi hicho na kupelekea kujengewa sanamu nje ya Uwanja wa Old Trafford akiwa na Denis Law na Sir Bobby Charlton, huku likitambulika kama The United Trinity. Best aliitumikia Manchester United kwa misimu 11, alifanikiwa kufunga mabao 137 katika michezo 361 huku akitumika katika nafasi za winga au kiungo

mshambuliaji. Pamoja na wachezaji hao kuandika historia kubwa ndani ya Manchester United wakivalia namba 7, hivi karibuni jezi hiyo imekuwa kituko ndani ya Old Trafford. Tangu kuondoka kwa Ronaldo ambaye alifanikiwa kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, hakuna mchezaji aliyefika hata nusu ya mafanikio yake licha ya Manchester United kufanya usajili wa gharama kubwa hivi karibuni. Baada ya Real Madrid kuvunja rekodi ya dunia kwa kumsajili

Mreno huyo, Manchester United ilimkabidhi jezi hiyo straika wa zamani wa Liverpool aliyetokea Newcastle United, Michael Owen ambaye aliivaa kwa misimu mitatu na kufanikiwa kupachika mabao matano katika michezo 31. Owen aliyetwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu England akiwa na Manchester United, aliondoka msimu wa 2012/13 alijiunga na Stoke City huku Antonio Valencia akirithi jezi namba 7. Licha ya winga huyo wa Ecuador kutambulika na jezi namba 25 alipojiunga na Manchester United mwaka 2009, alishindwa kufanya vizuri alipoanza kuvaa namba 7 katika msimu wa 2012/13, Valencia alifanikiwa kufunga bao moja tu kwenye michezo 30 aliyocheza msimu huo. Baada ya msimu kumalizika staa huyo aliyesajiliwa kutoka Wigan aliomba kurudishiwa jezi yake namba 25 ambayo anayo mpaka hivi sasa. Baadaye, Manchester United ilivunja rekodi ya usajili nchini England kwa kutoa kitita cha pauni milioni 59 kwa Angel Di Maria wa Real Madrid. Winga huyo wa Argentina alikabidhiwa namba 7 kutokana na uwezo aliokuwa

nao nchini Hispania, lakini hakufanikiwa kufanya vizuri akiwa na jezi hiyo. Di Maria alicheza michezo 27 katika msimu wake pekee wa 2014/15 ambao alifanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa asisti 10. Red Devils hawakukata tamaa walifunga safari mpaka Uholanzi ambako walimsajili kijana aliyekuwa moto wa kuotea mbali katika Ligi Kuu ya nchi hiyo, Memphis Depay. Lakini haikuwa bahati kwa Depay aliyecheza michezo 33 ya Ligi Kuu England na kufanikiwa kupachika mabao mawili tu. Mwishowe, aliamua kuondoka zake kutimkia Lyon ya Ufaransa ambako anafanya vizuri mpaka sasa ndani ya ligi hiyo. Msimu uliopita katika dirisha la Januari, Manchester United

walibadilishana wachezaji na Arsenal, walimtoa Henrik Mkhitaryan na kupewa Alexis

Sanchez aliyekuwa moto wa kuotea kwenye viunga vya Emirates. Majanga kwa

Sanchez yalianza alipojiunga na Red Devils huku akikabidhiwa jezi namba 7 ambayo haikuwa ishara nzuri kwake na waliopita hivi karibuni. Mpaka sasa amefanikiwa kucheza michezo 17 ya Ligi Kuu England akiwa Manchester United lakini amefunga mabao mawili na kutoa asisti nne za mabao. Hivi karibuni, kocha wa kikosi hicho, Jose Mourinho, alimpiga benchi katika michezo miwili iliyopita akimtaka staa huyo wa Chile kupandisha kiwango chake. Japo, inaaminika kufanya vibaya kwa Sanchez ni uchaguzi wa namba

mbali

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.