Yanga SC yamfunga mdomo Masoud Djuma

Dimba - - News - NA CLARA ALPHONCE

KOCHA Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, ni miongoni mwa viongozi wa benchi la ufundi wa timu hiyo walioonekana kuumizwa sana na jinsi washambuliaji wake walivyokuwa wakikosa mabao.

Kocha huyo aliyewapa furaha mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuonekana sambamba na Kocha Mkuu Patrick Ausemss, alionekana kuinuka na kushangilia kila mashambulizi yalipoelekezwa katika lango la Yanga.

Dimba Jumatano lilitaka kujua maoni yake juu ya kikosi chake ambacho licha ya kucheza vizuri lakini hakikufanikiwa kupata bao, lakini majibu yake yanaweza kukushangaza.

Kocha huyo alimjibu mwandishi wa gazeti hili kwamba, kamwe yeye hatazungumzia tena masuala yoyote yanayohusu soka katika maisha yake.

"Sitaki tena kuzungumzia masuala ya mpira, labda tuongee mambo yetu mengine," alisema kocha huyo.

Majibu hayo yanaashiria ni kama vile amezibwa mdomo kufuatia matokeo ya suluhu iliyopata timu yake, hasa kutokana na mashabiki wa Simba kudhani kwamba uwepo wake sambamba na kocha mkuu ungeleta ushindi mnono.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.