KLABU VISHALE ZAKUMBUSHWA USAJILI

Dimba - - News -

NA GLORY MLAY KATIBU Mkuu wa Chama cha Vishale Tanzania (TADA), Subira Waziri, amezikumbusha klabu za mchezo huo kuanza kujipanga na dirisha dogo la usajili ili kujiwinda na michuano ya Taifa Cup.

Michuano hiyo itashirikisha timu kutoka mikoa mbalimbali na imepangwa kuanza Novemba 23-25 hadi 30 mwaka huu, jijini Mbeya.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Subira alisema mbali na kufanya usajili, klabu hizo zinatakiwa kufanya uchaguzi ili kuendana na kalenda ya chama hicho.

Wachezaji wa timu ya Home Boys (jezi za njano), wakiwania mpira na wachezaji wa Super Eagle, wakati wa mchezo wa kombe la Mbuzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Feza Boys uliopo Kivule Dar es Salaam juzi. Picha na Jumanne Juma

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.