Julio atamba kutoa dozi FDL

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio', ametamba kikosi chake kitaibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Rhino Rangers utakaopigwa Jumamosi, Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Julio alisema, watapambana kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu ili kujiweka katika mazingira bora ya kutimiza ndoto za kucheza Ligi Kuu.

Alisema, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pamba FC katika mchezo uliopita, sasa nguvu zao wameelekeza dhidi ya Rhino Rangers.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.