MAUA SAMA AIVURUGA WCB

Dimba - - Burudani -

NA JESSCA NANGAWE NGOMA mpya ya msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama, inayojulikana kwa jina la ‘Iokote’, imeonekana kuzivuruga nyimbo mpya kutoka kwa mastaa wa lebo ya WCB.

Wimbo huo pamoja na kuingia kwenye matatizo baada ya kutumiwa vibaya na baadhi ya mashabiki wake hadi kutinga mahakamani, lakini umeonekana kuendelea kufanya vyema sehemu mbalimbali huku zile za mastaa wa WCB zikisahaulika.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Maua Sama alisema anashukuru kuona ngoma yake ikiendelea kupokelewa kwa ukubwa ambao hakuutarajia licha ya matatizo yanayomkabali.

Mastaa waliotoa nyimbo kutoka Kundi la WCB ni pamoja na Mbosso ambaye ametoa wimbo wa ‘Hodari’ Harmonize pamoja na Diamond ambaye ameshirikishwa katika wimbo wa ‘katika’ na kundi la Navy

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.