NINJA KWA KULA UROJO NI HATARI

Dimba - - Burudani - NA CLARA ALPHONCE

MIONGONI mwa wachezaji waliong’ara katika mechi ya mahasimu wa jadi kisoka, Simba na Yanga, yupo beki aliyegeuzwa kiungo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Mzanzibari huyo amekuwa na mwendelezo mzuri ndani ya kikosi cha timu hiyo tangu ajiunge nacho msimu uliopita, katika majukumu mapya ya kiungo mkabaji aliyopewa na kocha Mwinyi Zahera.

Kwa waliotazama mechi hiyo ya watani, Ninja alikuwa na jukumu la kufuta makosa yote ya mabeki wa timu hiyo mbele ya mastraika wa Simba waliokuwa na uchu wa kumtungua kipa, Beno Kakolanya.

Ikumbukwe beki huyo alitua Yanga akitokea JKU kama mrithi wa nahodha mstaafu wa timu hiyo ambaye kwa sasa ni meneja, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

DIMBA kupitia ukurasa wake wa nje ya soka limemvuta mezani na kupiga naye stori ili kujua maisha yake

nje ya uwanja. DIMBA: Unaishi wapi na nani? NINJA: Tabata na wachezaji wenzangu. DIMBA: Unapenda kula chakula gani? NINJA: Mchana napenda kula biriani na usiku lakini kila asubuhi huwa sikosi urojo kwani ni moja ya chakula ninachokipenda sana. DIMBA: Unapenda kinywaji gani? NINJA: Maji na juisi. DIMBA: Pesa (fedha) yako mara nyingi unatumia kwa matumizi gani zaidi?

NINJA: Kutunza familia yangu, wazazi wangu na pia kumsomesha mdogo wangu ambaye kwa sasa yupo chuo.

DIMBA: Vitu gani ni lazima uwe navyo kabla ya kutoka na marafiki zako?

NINJA: Mimi si mtu wa kutoka ‘out’ kabisa, napenda sana kupumzika.

DIMBA: Unapenda kuvaa mavazi ya aina gani?

NINJA: Simpo, mfano jinsi au pensi na tisheti tu.

DIMBA: Unapenda kukaa na washikaji wa aina gani na kupiga nao stori? NINJA: Wanamichezo wenzangu. DIMBA: Stori gani ambazo zikipigwa na washkaji kijiweni zinakuboa? NINJA: Kumjadili mtu kwa ubaya, dah.. yani sipendi na ninaondoka kabisa sehemu hiyo. DIMBA: Kitu gani huwezi kusahau tangu mwaka huu uanze? NINJA: Michuano iliyopita Kombe la Mapinduzi, kwani ilinisababishia majeraha ambayo yalinifanya nikae miezi mitatu nje. Majeraha hayo nilipata dakika ya pili tu ya mchezo dhidi ya Mlandege. DIMBA:

Kitu gani huwezi kufanya kwenye maisha yako? NINJA: Kumdharau mtu. DIMBA: Kati ya nguo na viatu ni kipi ambacho umenunua bei ghali? NINJA: Kiatu cha mpira nimenunua dola 1000. DIMBA: Maswali gani ambayo hupendi kuulizwa na mashabiki zako? NINJA: Mbona siku hizi huchezi, tena utakuta mtu anakuuliza kwa kukusanifu akimaanisha kuwa kiwango kimeshuka ndio maana sichezi, wakati anatakiwa kuuliza vizuri na kujua tatizo. DIMBA: Unapenda kuvaa mavazi ya kampuni gani? NINJA: Nike kwa sababu ni kampuni inayowavalisha wachezaji ninaowapenda. DIMBA: Unapenda kuendesha gari ya aina gani? NINJA: Prado DIMBA: Unavutiwa na mwanamke wa aina gani? NINJA: Mstaarabu anayejistiri, mwenye tabia njema na anayemjua Mungu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.