NINJA ALIANZA NA HILI ‘KARIAKOO DERBY’

Dimba - - Burudani -

WAKATI Ibrahim Ajib wa Yanga akiacha gumzo mchezo wa watani wa jadi, Simba dhidi ya Yanga baada ya kupiga mpira nje tofauti na ilivyozoeleka, beki wake, Abdallah Shaib ‘Ninja’, alikuwa mchezaji wa kwanza kuonywa na mwamuzi. Ninja alikuwa sehemu ya mabeki watano wa Yanga likiwa ni wazo la kocha Mwinyi Zahera kuwazuia mastraika wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere, Emmanue Okwi na baadaye Adam Salamba. Beki huyo wa kati anayevalia jezi namba 23, alijikuta akiwa wa kwanza kuonywa kwa maneno na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukya, baada ya kuonekana kucheza faulo mbaya mbili dakika za mwanzo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.