DAKIKA 80 ZA CHAMA HAZIKUMWACHA SALAMA YONDANI

Dimba - - Burudani -

KINGO mpya wa Simba, Clatous Chama, alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliong’ara katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliowakutanisha na watani zao wa jadi, Yanga. Mzambia huyo aliyecheza jumla ya dakika 80 kabla ya kumpisha Said Ndemla, alikuwa ametengeneza muunganiko wa aina yake eneo la kiungo alipokuwa sambamba na kina Jonas Mkude pamoja na James Kotei. Mbali na muunganiko wao kuwanyanyasa zaidi wapinzani wao, Papy Tshishimbi na Feisal Salum, lakini pia Chama alikuwa kikwazo kwa Kelvin Yondani ambaye alijikuta akionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea Mzambia huyo faulo tatu kwa nyakati tofauti.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.