Kocha Simba amfungia kazi Okwi

Dimba - - News - NA CLARA ALPHONCE

KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na Straika wa Kiganda, Emmanuel Okwi, kwenye Ligi Kuu msimu huu, kimeendelea kuzidi kumpasua kichwa Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems.

Ikumbukwe Okwi ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita, baada ya kufunga mbao 20, lakini msimu huu mpaka sasa ameshindwa kutupia bao hata moja kati ya michezo mitano aliyocheza.

Aussems alikiri kushuka kwa kiwango cha Okwi na kudai kuwa atalifanyia kazi suala lake.

ìOkwi hajapafomu vizuri katika mchezo wa Simba na Yanga, lakini hiyo ni kawaida kwa mchezaji, lakini natakiwa kulifanyia kazi suala hilo ili aweze kufanya vizuri katika michezo iliyobaki,î alisema Aussems.

Tayari mastraika wenzake wanaocheza nao ambao ni Meddy Kagere na John Bocco wamefanikiwa kufunga mabao kwenye Ligi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.