Kiluvya yaipania Mawenzi Market leo

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

KOCHA Mkuu wa timu ya Kiluvya United, amewaonya wapinzani Mawenzi Market wasitegemee kupata mteremko kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Daraja la Kwanza utakaopigwa leo Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Akizungumza na DIMBA, Kocha Mkuu wa Kiluvya, Yahaya Issah, alisema wapo katika maandalizi makali kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mechi yao ili wajiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Alisema ameshafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita na anaamini kila mchezaji atatimiza majukumu yake vyema uwanjani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.