Magongo walia ubovu wa viwanja

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es Salaam (DRHA), Mnonda Magani, amesema changamoto inayowakabili kwa sasa ni ukosefu wa viwanja vya kufanyia mashindano.

Akizungumza na DIMBA, Magani alisema wanapata matatizo ya viwanja kutokana na vinavyotumika kujaa mashimo na kuwafanya wachezaji washindwe kucheza.

“Changamoto ya viwanja ni tatizo kubwa kwetu hasa kwa wakati huu ambao wachezaji ni wengi, vinavyotumika kwa sasa havina ubora kwa sababu vimejaa mashimo,” alisema.

Magani aliiomba Serikali kuwatengenezea maeneo yao kwa sababu wachezaji ni wengi lakini pia wanaendelea kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.