Krish wa Uwoya alivyomkumbuka marehemu baba yake

Dimba - - Nyuz Nyuz -

MTOTO wa Irene Uwoya aitwaye Krish, amemkumbuka baba yake mzazi, marehemu Hamad Ndikumana, aliyefariki ghafla Novemba 15, 2017 na juzi ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Ndikumana na hivyo amemwandikia ujumbe wa kumkumbuka.

Uwoya ametumia ukurasa wake wa instagram kuonyesha barua aliyoiandika Krish kwa baba yake na kusema kuwa, amemkumbuka sana na hakutaka baba yake afariki na mwisho wa ujumbe huo alimalizia kwa kusema anamtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Ujumbe wa Lulu baada ya kuvishwa pete

MAPEMA mwanzoni mwa juma hili zilisambaa picha za msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael, zikionyeshwa akivishwa pete na mchumba wake, Majizo.

Baada ya kusambaa kwa picha hizo, wapo waliodhani huenda anaigiza, lakini mwenyewe akaamua kuvunja ukimya na kuweka picha yake akiwa na mchumba wake huyo na kuandika: "Kwa dhati tunapendana filamu hatuigizi, nyota zetu zafanana kutuchafua hamuwezi."

Uwoya ajipa jina la ëMama mifugoí

STAA wa filamu nchini, Irene Uwoya, wiki hii ameonekana kuzungumziwa sana, hii ni mara baada ya kupostI picha akiwa kwenye zizi la ngíombe na kuandika ujumbe ambao umewashangaza wengi, huku wakiamini ameamua kubadilisha aina ya kujiingizia kipato.

Uwoya alitupia picha akiwa kwenye zizi la ngíombe huku akiwa kashikilia zana za kazi na kuandika: "Mama mifugo nikiwa kazini. Kupambana si lazima uwe kazini au ofisini na duka...njia zipo nyingi sana, pambana."

Kotei kamuomba radhi Gadiel hivi

JUMAPILI ya Septemba 30 ulichezwa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga na gemu hiyo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare tasa, na moja ya tukio lililoteka mashabiki ni kiungo wa Simba raia wa Ghana, James Kotei, kumpiga mgongoni beki wa Yanga, Gadiel Michael, na tukio hilo kunaswa na kamera za Azam TV.

Kotei kupitia ukurasa wake wa Instagram kaamua kuomba radhi na kuandika hivi: "Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa mchezaji mwenzangu kwa purukushani iliyojitokeza kwenye derby na ninaungana na wanamichezo kukemea kitendo hicho kisichokuwa cha uanamichezo.

Dogo Janja anahitaji mwanasaikolojia

INASEMEKANA Dogo Janja hayuko sawa kisaikolojia, hii ni baada ya kupost picha kupitia ukurasa wake wa instagram akiwa na mwanasaikolojia maarufu nchini, Chris Mauki.

Wengi wamedai sababu ya Dogo Janja kukutana na mwanasaikolojia huyo ni kuwekwa sawa yale yote anayopitia kwa sasa kutokana na wengi kuhusisha kuwa kuna ugomvi unaendelea kati yake na mke wake, Irene Uwoya, kitu hicho kinamfanya asiwe katika hali yake ya kawaida. Shukrani sana kaka...ni furaha kuwa na watu kama nyinyi.

Kanye West katoa Bil.2 Kardashian alinde penzi

RAPA Kanye West imemlazimu kumlipa mke wake, Kim Kardashian, dola milioni 1, ambayo ni sawa na Sh bilioni 2 baada ya kumzuia mke wake kuposti picha moja ya tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kim akiwa kwenye mahojiano ya uzinduzi wa Podcast ya mtangazaji amesema kuwa wiki moja kabla ya Siku ya Mama Duniani alitafutwa na kampuni kubwa ya mavazi nchini Marekani ikimtaka aposti picha moja ya tangazo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na itamlipa dola laki 9, lakini ilimpasa aombe ushauri kwa mumewe, ambaye alimkatalia kufanya hivyo.

Diamond kula 'birthday' baharini

KUHUDHURIA 'birthday' ya Diamond ni Sh milioni 1. Mapema wiki hii staa wa Bongo Fleva, Diamond alitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa, huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa hatua hiyo. Diamond amekuwa na tabia ya kusherehekea siku yake hiyo muhimu kwa aina tofauti na safari hii ameamua kusherehekea leo Oktoba 7, ambayo itafanyika ndani ya boti huku kiingilio kikiwa dola 500, sawa na zaidi ya shilingi milioni 1, ambayo itahudhuriwa na watu mashuhuri ambao watakuwa wamevalia mavazi meupe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.