PRISONS YAISUKUMA NDANI MBEYA CITY

Dimba - - Mbele - CLARA ALPHONCE NA SAADA SALIM

KAULI ya kaimu Rais wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah, maarufu kama Try Again, kwamba suala la Masoud Djuma, kubakia kwenye Klabu hiyo halina afya, ni dhahiri Mrundi huyo ameshafungashiwa kila kilicho chake na sasa anayekuja kurithi mikoba yake ameshajulikana.

Akizungumza jana asubuhi na kituo cha Azam TV, Try Again alikiri kwamba kuna hali ya sintofahamu kati ya Djuma na Kocha Mkuu Patrick Aussems, na kwamba watatangaza maamuzi magumu muda wowote.

Alisema, Djuma amekuwa hana mawasiliano mazuri na Aussems, jambo ambalo limepelekea kuleta msuguano usiokuwa na tija, pia akikumbushia namna kama hiyo alipokuwa na kocha mwingine, Pierre Lechantre.

"Ni kweli kumekuwa na matatizo ambayo yamekuwa yakijirudia baina ya Masoud Djuma na benchi la ufundi, haswa kwa makocha wakuu, akiwamo Joseph Omog na Pierre Lechantre aliyeondoka.

“Tumekuwa tukifanya jitihada za kutatua tatizo hilo bila mafanikio, siwezi kueleza mengi kwa sasa, ila tutakuja na tamko rasmi baadaye, tunachoweza kusema ni kuwa suala la Djuma kubaki Simba halina afya nzuri", alisema.

Bosi huyo wa Simba ameeleza kuwa, hawezi kufukua kila kitu kwa sasa mpaka hapo baadaye kama klabu watakapokuja kuweka wazi mwafaka wa sakata hilo ili kusuluhisha kwa faida na maslahi mapana ya klabu.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa, uongozi ni kama umeshafikia maamuzi ya kuachana na Mrundi huyo ili kumwachia Kocha Mkuu aendelee na mipango yake kwa uhuru zaidi.

Taarifa zaidi kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi zinadai kuwa, anayepigiwa hesabu za kurithi mikoba yake ni kocha Mkuu wa Mbao FC, Amri Said, kutokana na uzoefu alionao.

“Kuna kila dalili kwamba Amri Said, akakabidhiwa jukumu hilo la kuwa kocha msaidizi na kuchukua nafasi ya Djuma, Amri ni mzoefu na amekuwa kocha msaidizi kwa nyakati tofauti ndani ya Klabu, ndiyo maana watu wanamfikiria yeye,” alisema kigogo mmoja.

Dimba lilimtafuta Amri Said ili kujua ukweli wa tetesi hizo, alidai naye anasikia taarifa hizo, hivyo anasubiri waje rasmi mezani ili kuzungumza.

“Mimi kazi yangu ni ukocha, Simba ni klabu kubwa, wakinifikiria kuchukua mikoba ya Djuma sitaiacha, nina imani nitaisaidia, kwani haitakuwa mara ya kwanza kusimama kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

“Nimefanya kazi na makocha wengi ndani ya Simba, akiwamo Cirkovic Milovan, Patrick Phiri na tulipata mafanikio makubwa miaka hiyo ya 2010, najiamini na naamini kile ninachokifanya,” alisema.

Mbali na Amri, mwingine anayetajwa ni Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola, ambaye alipoulizwa alisema yeye hana taarifa hizo.

“Sina taarifa yoyote juu ya suala hilo, ndio kwanza nasikia kwako, kwani Simba wanamfukuza Djuma? Mimi sijui bwana,” alisema Matola kwa kifupi.

Taarifa nyingine zinadai kuwa, tayari Djuma ameshaingia kwenye rada za Klabu ya AFC Leopards ya nchini Kenya, na huenda akalamba mkataba wa maana.

Leopards imemfuta kazi kocha wake mkuu, Robert Matano 'The Lion', baada ya wenye timu yao kutokurithishwa na matokeo mabaya mfululizo ambayo wamekuwa wakiyapata katika michuano ya Ligi Kuu nchini humo, maarufu kama KPL.

Mbali na Djuma, pia kuna Watanzania wawili, Denis Kitambi ambaye kwa sasa anafundisha Klabu ya Sai Sporting Club ya Bangladesh na Hemed Morocco (Kocha wa Singida United na msaidizi wa Taifa Stars), wanaotajwa kuchukua nafasi ya Matano kutokana na rekodi zao nzuri.

DIMBA lilimtafuta Mwenyekiti wa Leopards, Daniel Mule, ambaye alikiri kuwapo katika mipango ya kuajiri kocha mwingine, huku akidai kuwa sasa hawahitaji tena kocha Mzungu, bali jicho lao watalielekeza kwa makocha wa Kiafrika.

“Tunamaliza ligi kesho (leo), hivyo keshokutwa tutakuna na Bodi ya Timu pamoja na benchi la ufundi, kwa ajili ya kuangalia mchakato wa kutafuta mwalimu atakayerithi nafasi ya Matano pamoja na suala zima la usajili.

“Kwa sasa tunahitaji kocha Mwafrika ambaye ana jina kubwa kulingana na ukubwa wa timu yetu, lakini pia tunahitaji mwenye uzoefu kwa sababu sasa tunahitaji kujipanga ili kufanya vizuri msimu ujao.

“Mpaka sasa Kitambi (Denis), amekuwa akitajwa sana, sababu ni maelewano mazuri aliyokuwa nayo pamoja na kutengeneza timu yetu, ikifanya vizuri, lakini pia hajaondoka kwa ubaya alikubaki kwa wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki, hata hivyo ikishindikana kwake bado kuna wengine tumewaona,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.