Singida United yaishusha Azam FC

Dimba - - News - NA CLARA ALPHONCE

LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea tena jana kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini, huku Mtibwa Sugar wakiendelea kushikilia usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar, ambao jana walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam, wameendelea kukaa kileleni baada ya kufikisha pointi 17, katika michezo 9 ya Ligi Kuu waliyocheza.

Singida United nao wamepaa kutoka nafasi ya sita hadi nafasi ya pili na kumshusha Azam FC, waliolingana kwa pointi, lakini akimshinda kwa mabao ya kufunga.

Simba wa nyikani hao walifanikiwa kuchukua nafasi hiyo baada ya jana kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua, Singida.

Mchezo mwingine ambao ulivuta watu jana ni ule derby ya Mbeya iliyowakutanisha Tanzania Prisons dhidi ya Mbeya City na mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa bao 2-1 waliopata Mbeya City.

Ruvu Shooting wao walishindwa kutamba mbele ya wanyeji wao, Kagera Sugar, baada ya kumaliza dakika 90 kila timu ikiwa haijaona lango la mwenzake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.