TIGER WOODS

AVURUNDA TENA RYDER CUP 2018

Dimba - - Showbiz -

MKONGWE wa mchezo wa gofu duniani, Tiger Woods, ametajwa kuwa ndiye mchezaji mwenye takwimu mbovu zaidi kuliko wachezaji 24 walioshiriki michuano ya kuwania taji la Ryder 2018.

Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo iliyofanyika jijini Paris na kushuhudiwa timu kutoka Bara la Ulaya zikiibuka na ubingwa mbele ya timu kutoka Marekani, Woods alionesha kupania kufanya vyema mwaka huu.

Lakini baada ya siku tatu za mashindano hayo, Woods alijikuta akimaliza kwa kiwango kibovu, baada ya kucheza jumla ya mechi nne na zote alikutana na vichapo.

Kiujumla, rekodi ya Woods katika mashindano yote ya Ryder Cup aliyoshiriki inaonesha alishinda mechi moja tu mwaka 1999, na amekutana na jumla ya vipigo saba.

Aidha, kwa kiwango alichokionesha katika michuano hiyo ya mwaka huu, ni wazi Woods bado hajaielewa kabisa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.