Seagal asusa kipindi kisa swali la ubakaji

Dimba - - Showbiz -

SWALI la mwandishi wa kituo cha BBC kuhusu madai ya ubakaji yanayomkabili Steven Seagal, limemfanya mwigizaji huyo maarufu wa Marekani kususia mahojiano yake hayo na ‘kusepa zake’.

Ishu ilikuwa hivi, mapema wiki hii, Seagal alikuwa kwenye kipindi hicho maalumu na mtangazaji, Kirsty Wark, ambaye alimuuliza mkali huyo akitaka kujua anayachukuliaje madai hayo, swali ambalo lilimchefua mwigizaji huyo na kuamua kususia kipindi.

Hata hivyo, Seagal aliwahi kukanusha madai hayo ambayo yaliibuliwa Machi mwaka huu na kimwana Regina Simons, ambaye alidai mkali huyo wa filamu za mapigano alimbaka akiwa na umri wa miaka 18.

Mwingine aliyeibua madai ya kunyanyaswa kijinsia na Seagal ni Faviola Dadis, ambaye alisema wakati wakiwa katika eneo la kuigiza, mwigizaji huyo alimfanyia vitendo vya unyanyasaji.

Hata hivyo, Mwanasheria wa Seagal, Anthony Falangetti, alikanusha madai hayo katika mahojiano yake na Kituo cha ABC News.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.