STRAIKA BRIGHTON ASAKA REKODI YA HARRY KANE

Dimba - - Dimba Special -

STRAIKA wa Brighton, Glenn Murray, mbali ya kuiwezesha timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi West Ham, mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa usiku wa Ijumaa, lakini pia bao alilofunga linamfanya kusogelea rekodi ya Harry Kane wa Tottenham. Lilikuwa ni bao lake la 12 kwenye Premier League tangu kuanza kwa mwaka huu 2018, ambapo rekodi hiyo inashikiliwa na Mwingereza mwenzake, Harry Kane (17), akifuatiwa na Jamie Vardy (14). Kwa upande mwingine, West Ham ikiwa chini ya makocha tofauti, Slaven Bilic, David Moyes na Manuel Pellegrini, walikuwa wanapoteza mchezo wa tatu wa ligi mbele ya Brighton.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.