MESSI

ANAJUA KUWA MACHOZI NA MAUMIVU VINA UHUSIANO

Dimba - - Dimba Special -

KILA ninapomtazama Lionel Messi, nakumbuka ahadi aliyoiweka mbele ya mashabiki wa Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou mwanzoni mwa msimu huu wakati anakabidhiwa kitambaa cha unahodha.

Messi hakuwa na kingine zaidi ya kuwaambia mashabiki wa Barcelona watarajie kuliona taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja huo, baada ya miaka mitatu kupita.

Ndiyo, mara ya mwisho Barcelona wanashinda taji hilo safu yao ya ushambuliaji ilikuwa na watu watatu makini, Messi, Neymar na Luis Suarez.

Uhakika wa kushinda michezo yao ulikuwa mkubwa zaidi hata kabla hawajaingia uwanjani, ulikuwa utatu ambao ulifanya maisha yaonekane rahisi ndani ya Camp Nou.

Ubora wa Real Madrid ulifunika kila kitu kilichopo Barcelona na kuwaongezea njaa ya kuhitaji zaidi kushinda taji hilo.

Iko hivi, kwa misimu mitatu mfululizo Barcelona waliishia katika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu wa 2015/16, walitolewa na Atletico Madrid katika hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 3-2, Barcelona walishinda 2-1 mechi ya kwanza, lakini ya pili waliruhusu kupigwa mabao 2-0.

Msimu wa 2016/17, Barcelona walikumbana na kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Juventus na kuishia katika hatua ya robo fainali kwa mara ya pili mfululizo.

Na msimu uliopita ambao ulikuwa na kumbukumbu kwa AS Roma kwa kuiondoa Barcelona kwa idadi ya mabao ya ugenini baada ya michezo miwili kumalizika kwa sare ya 4-4.

Lakini mabingwa hao wa Hispania walianza kwa ushindi wa mabao 4-1 na mechi ya pili ilimalizika kwa Roma kushinda mabao 3-0.

Hayo yote yalikuwa maumivu kwa Messi, sura yake haikutoa machozi, lakini moyo wake ulikuwa katika maumivu makubwa kutambua kuwa dunia yote inamwangalia, ukizingatia upande wa pili Real Madrid walikuwa moto wa kuotea mbali.

Kwa upande wa Ligi Kuu Hispania, Barcelona kwa misimu mitatu wametwaa mataji mawili, huku hawana njaa kama ilivyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Messi anaamini Barcelona ni timu inayostahili kushinda taji la Ulaya kila msimu, kauli yake pale Camp Nou haikuwa ya bahati mbaya au kufurahisha mashabiki tu.

Kitambaa cha unahodha kinatufanya tumuone Messi mpya ambaye labda aliishia nyuma ya kivuli cha akina Carlos Puyol, Andres Iniesta au Xavi Hernandez.

Unapokabidhiwa kitambaa maana yake timu yote ipo nyuma yako, unahodha wa kipindi hiki unalenga zaidi kwa wachezaji nyota ambao ni taswira ya klabu husika au kibiashara inakuwa inavutia tofauti na miaka ya nyuma.

Katika michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa mpaka sasa, Messi kafanikiwa kufunga mabao matano, bao moja pungufu katika yale aliyofunga msimu uliopita wote.

Messi kuwa katika kiwango cha juu mwanzoni mwa msimu kunatoa taswira ya timu hiyo kuwa kwenye wakati mzuri wa kutwaa mataji msimu huu.

Messi amejiweka kundi tofauti na wenzake, japo wote wanaishi katika ndoto moja ya kuhitaji kushinda taji hilo kubwa Ulaya.

Malengo ya Messi yaliambatana na ahadi ambazo aliziweka pale Camp Nou, kwa kiasi kikubwa hata wachezaji wenzake watakuwa na nguvu za kupambana kila watakaposhuka dimbani wakitambua kuwa nahodha aliweka ahadi.

Kushi nda taji la mabingwa Ulaya si rahisi, lakini inahitaji mwendelezo wa ubora wa kila mmoja kutoka mchezo mmoja mpaka mwingine.

Ndiyo iko hivyo, tazama mabingwa wote walioshinda taji hilo zaidi ya kuwa na uhakika wa kushinda michezo yao wanapoingia uwanjani.

Kwa namna moja au nyingine, wachezaji wa Barcelona hawana uwezo mkubwa sana, lakini wanaweza kujitoa kupigana kwa kila kitu sababu Messi amekuwa mstari wa mbele na muwazi juu ya ndoto zake. Safari ya mafanikio ya Barcelona msimu huu ilianzia katika kauli ya Messi, achana na mambo mengine ya mashabiki kuhitaji kocha wa kikosi hicho, Ernesto Valverde, aondoke kutokana na mpira

unaochezwa na timu hiyo. Inawe zekana Messi alisimama mbele ya kioo na kujitazama kila wakati, misimu mitatu bila taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ni tatizo kwake. Kaamua kubeba msalaba mzito mbele ya wengine ambao wanafuata mkumbo huo kwa kujitolea kutimiza ndoto za timu nzima labda bila kujua wanachokifanya. Kwa namna moja au nyingine, machozi na maumivu ambayo yapo katika moyo wa Messi yanapelekea ulimwengu kumuona akiwa mpya na mwenye njaa ya kuhitaji kufanikiwa zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.