JE WAJUA?

Huyu ndiye Cristiano Ronaldo usiyemfahamu

Dimba - - Dimba Special -

Akiwa na rekodi hiyo ya usajili, siku ya utambulisho wake ndani ya klabu hiyo kubwa nchini Hispania.

KIPINDI hiki ni kigumu kwa nyota mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo, ambaye amefunguliwa kesi kwa kosa la kubaka na mwanadada, Kathryn Mayorga, walipokutana mwaka 2009 Las Vegas, Marekani.

Mayorga alibainisha kuwa Ronaldo alimlazimisha kufanya naye mapenzi wakati akibadilisha nguo, huku akikataa kufanya kitendo hicho, na mwishowe nahodha huyo wa Ureno kuamua kumbaka.

Mwanadada huyo alitoa taarifa ya kubakwa kwenye kituo cha polisi ndani ya mji huo, lakini hakumtaja jina ambaye alifanya kitendo hicho.

Oktoba 3, Ronaldo kupitia mitandao yake ya kijamii aliandika kuwa kuna watu wanatumia jina lake kupata umaarufu na kusema kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho kama ilivyoelezwa.

Tangu ajiunge na Juventus, Ronaldo amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo ya Ligi Kuu Italia, Serie A msimu huu.

Kabla ya kuanza kufunga mabao, Ronaldo alikuwa kwenye juhudi kubwa za kutafuta mabao, lakini mambo hayakuonekana kumwendea kama alivyotaka.

Pamoja na kufanya juhudi kubwa za kuhitaji kukwamisha mpira wavuni katika nyavu za wapinzani, staa huyo raia wa Ureno aliongoza kwa kupiga mashuti mengi zaidi ya mchezaji yeyote Italia, lakini hakufanikiwa kufunga bao, alipiga mashuti 26.

Hivi karibuni Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, alisema kuwa, anaamini hilo jambo haliwezi kumsumbua Ronaldo, ambaye anajua nini anakifanya awapo uwanjani, huku akisisitiza kuwa staa huyo wa Ureno atakuwa hatari zaidi kama akifanikiwa kufunga bao la kwanza, sababu atahitaji kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Ronaldo ni miongoni mwa nyota wanaoangaliwa zaidi ulimwenguni kutokana na kile anachokifanya awapo ndani ya uwanja, pia ni mmoja wa wachezaji bora kwa zaidi ya miaka 10.

Pamoja na yote hayo kumtokea staa huyo wa zamani wa Real Madrid, kuna baadhi ya mambo inawezekana ukawa huyajui kabisa kuhusu nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno.

AIKATAA JEZI NAMBA 7

CR7, Manchester namba Hivi Lisbon. lakini Wakati sasa 28, Ronald dunia kama Unit huo inamfahamu kama o aliposajiliwa na d alihitaji kuvaa jezi ilivyokuwa Sporting akiwa na miaka 18, hamu jezi namba saba aliwa na wachezaji mkubwa ndani ya United kama George ntona na David ocha wa Manchester Alex Ferguson, hi Ronaldo kuvaa kiamini ana uwezo dea haki kama nya akina Beckham. wa siku kila kitu kuwa historia. alikuwa ilikuwa anafa imev wenye uwez Manchester Best, Eric C Beckham. Lakini K United, Sir alimshawi jezi hiyo a wa kuiten walivyof Mwisho kiligeuk

AFYA MGOGORO, ASINGECHEZA SOKA

Ronaldo ni mfano kwa wachezaji wengi wa sasa wanaochipukia kutokana na uwezo mkubwa alionao wa kufanya mazoezi yaliyomfanya kuwa na kasi, nguvu na imara. Hilo si geni kwa wengi wanaomfahamu staa huyo, lakini wakati akiwa na miaka 15 alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mapigo ya moyo kudunda kwa kasi zaidi ya kawaida. Katika mahojiano, mama yake, Maria Dolores Aveiro, alibainisha kuwa mwanawe asingekuwa mchezaji soka sababu ya tatizo hilo la moyo.

AVUNJA REKODI YA MARADONA

Baada ya kuitumikia Manchester United kwa miaka sita, mwaka 2009 Ronaldo alijiunga na Real Madrid kwa dau la pauni milioni 80, akiweka rekodi ya uhamisho ghali zaidi ulimwenguni.

Akiwa na rekodi hiyo ya usajili, siku ya utambulisho wake ndani ya klabu hiyo kubwa nchini Hispania aliweka rekodi nyingine ya kuangaliwa na mashabiki 80,000 waliojitokeza siku hiyo katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Ronaldo alivunja rekodi ya Diego Maradona, ambaye aliangaliwa na mashabiki 75,000 katika Uwanja wa San Paolo, akiribishwa na mashabiki hao mwaka 1984.

AITWA MTOTO ANAYELIA

Siyo siri tena, Ronaldo hujitolea zaidi pindi anapokuwa na jezi ya timu yake awapo ndani ya uwanja, suala la kulia linaonekana kuwa ni tabia yake.

Ricardo Santos ni mmoja wa marafiki wa karibu wa mchezaji huyo, alibainisha kuwa wakati wa udogo wao, Ronaldo alikuwa anapenda sana kulia.

Wakati huo wakiwa katika timu ya Andorinha, usipompigia pasi au timu ikifungwa alikuwa anaangua kilio na kupelekea wenzake kumpachika jina la ‘mtoto anayelia’.

ANGEKUWA MCHEZAJI WA BARCELONA

Jambo moja ambalo itakuwa umelifikiria kwa haraka ni uwepo wa Lionel Messi na Ronaldo katika kikosi kimoja cha Barcelona. Lakini kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 kumekuwa na upinzani mkubwa kati ya wachezaji hao wawili, huku kila shabiki akitamani siku moja kuona nyota hao wanacheza katika kikosi kimoja. Ukirudi nyuma miaka 15 iliyopita, rais wa Barcelona wakati huo, Joan Laporta, alibainisha kuwa mwaka 2003 alipewa nafasi ya kumsajili Ronaldo kutoka Sporting Lisbon kwa ada ya euro milioni 17. Lakini rais huyo tayari alikuwa ameshafanya usajili wa Ronaldinho, Ricardo Quaresma na Rafael Marquez, kwa hiyo asingeweza kuongeza mchezaji mwingine ndani ya kikosi hicho. Baada ya hilo kutokea ilishuhudiwa Ronaldo akijiunga na Manchester United na hapo baadaye wapinzani wakubwa wa Barcelona, ambao ni Real Madrid.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.