Kumbe michezo ya wanawake inafuatiliwa aisee

Dimba - - Dimba Special -

UTAFITI mpya wa kimataifa umebaini asilimia 84 ya mashabiki wa michezo ñ zaidi ya nusu ambayo ni wanaume ñ wanashawishika kufuatilia michezo inayochezwa na wanawake.

Katika utafiti huo uliofanywa na Nielsen Sports nchini Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Australia na New Zealand, ripoti inaonyesha asilimia 51 ya mashabiki wanaume wanajihusisha na michezo ya wanawake. Aidha, jumla ya idadi ya watu ñ wanaume kwa wanawake ñ katika nchi nane, asilimia 64 wana hamu kufuatilia angalau mchezo mmoja wanaocheza wanawake. Hata hivyo, ufuatiliaji unakuwa mkubwa zaidi katika michezo ambayo inashirikisha wanaume na wanawake kwa wakati mmoja ñ mfano riadha au tenisi ñ kinyume cha inapofanyika tofauti kama vile gofu, kriketi au soka. Utafiti ambao ulihusisha watu 1,000 kutoka kila nchi, pia ulibaini michezo ya wanawake inaonekana zaidi kuwa na ëushawishií, ëmaendeleoí, ëchimbuko la familiaí na ësafií kuliko michezo ya wanaume inayoonekana kuweka mbele ëfedhaí. Takribani asilimia 50 ya wanawake wanafikiria michezo ya wanawake ina ushindani ikilinganishwa na asilimia 44 ya wanaume, wakati asilimia 41 ya wanawake na asilimia 31 ya wanaume wanadhani ina ushawishi.

* Nini kingine utafiti ulibaini?

Licha ya medali kibao za dhahabu za Olimpiki, Serena Williams, Jessica Ennis-Hill na Laura Kenny nini kinachowafanya kuwa sawa. Jibu: Ni wanamichezo wanaotambulika zaidi kwa umati wa Uingereza, kwa mujibu wa utafiti wa Nielsen Sports. Wanaoongoza kwa wachezaji wa timu za wanawake ni nahodha wa Manchester City na England, Steph Houghton na mabingwa wa Kombe la Dunia mchezo wa kriketi, Heather Knight na Anya Shrubsole. Wakati hamu ya soka la wanawake ikiwa ni asilimia 43, takwimu hiyo ni sawa na idadi ya watu milioni 105 kutoka nchi nane. Ufaransa watakuwa wenyeji wa Kombe la Dunia kwa wanawake 2019 na wakati asilimia 63 ya watu wanaelewa michuano hiyo mwakani, utafiti umebaini ni asilimia 34 tu ndio wana hamu ya michuano hiyo, ikilinganishwa na asilimia 45 waliofuatilia Kombe la Dunia kwa wanaume mwaka huu. Takribani nusu ya asilimia 43 ya jumla ya idadi ya watu kutoka nchi nane walisema watakwenda kushuhudia moja kwa moja michezo ya wanawake, ikilinganishwa na asilimia 63 watakaofanya hivyo kwa michezo ya wanaume.

JESSICA ENNIS-HILL

SERENA WILLIAMS

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.