Lucas Eden Hazard, Moura

Ryan Fraser hawakamatiki Ligi Kuu England

Dimba - - Sport Pesa - LONDON, England

KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard, sambamba na Lucas Moura (Tottenham) na Ryan Fraser kutoka AFC Bournemouth, wanatajwa kuwa ni nyota tishio kwa sasa Ligi Kuu England, kwa mujibu wa Mtandao wa Sky Sports. Hatua hiyo inatokana na utendaji kazi wa nyota hao walichokifanya uwanjani tangu kuanza kwa msimu huo mpya kwa namna wanavyovisaidia vikosi vyao kupata matokeo bora. Nyota wengine wanaotajwa kufanya vizuri ni Sergio Aguero (Manchester City), James Maddison (Leicester City) ambaye amemshawishi hadi kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate kumjumuisha kikosini. Mbali na hao, lakini katika hiyo orodha yapo majina ambayo yanaonekana kuwa ‘surprise’: Jose Holebas (6), Ryan Fraser (10) na Joao Moutinho (15).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.