Jurgen Klopp: Man City ni ‘muziki mnene’

Dimba - - Sport Pesa -

"Man City ni timu imara sana yenye muunganiko wa kuridhisha, ina pesa za kutosha, lakini pia wana kocha bora,

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, anaamini Manchester City ni miongoni mwa timu bora sana duniani, hasa msimu huu ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi hiyo inayofuatiliwa na idadi kubwa ulimwenguni kote.

Wawili hao wanatarajia kushuka dimbani kuvaana mchezo wa Ligi Kuu England ‘Super Sunday’, unaotarajiwa kupigwa jioni ya leo Uwanja wa Anfield.

Klopp anasema Man City wako vizuri kuanzia masuala ya kiuchumi, utawala bora, lakini pia wana bechi bora la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mhispania, Pep Guardiola.

"Man City ni timu imara sana yenye muunganiko wa kuridhisha, ina pesa za kutosha, lakini pia wana kocha bora, utakuwa ni mchezo mzuri wa kuushuhudia,” anasema Mjerumani huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.