Ni sahihi kumlaumu kocha wa Stars kutomuita Ajib kikosini?

Dimba - - Burudani Za Wasanii -

JUMAPILI iliyopita kulikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Mbao FC ya Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa Wanajangwani hao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Shukrani za kipekee kwenye ushindi huo ziende kwa straika Ibrahim Ajib wa Yanga, ambaye alitoa pasi ya mwisho ya bao la kwanza lililofungwa na Raphael Daudi na pia kuifungia timu hiyo bao la pili.

Bao hilo alilolifunga kwa ustadi wa hali ya juu, limezua mijadala sehemu mbalimbali juu ya mchezaji huyo kuonyesha kiwango bora kwa timu yake tangu msimu huu, lakini cha kushtua kocha wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Amunike, ameshindwa kumuita kwenye timu hiyo.

Hadi sasa Ajib ameshaifungia Yanga mabao mawili, huku akitoa pasi za mwisho za mabao (assist) sita kwa michezo sita waliyocheza.

Licha ya kuonekana kutoa mchango huo mkubwa kwenye klabu yake, lakini jicho la Amunike limeshindwa kumuona mchezaji huyo, huku wengi wakiona kama amemkosea.

Ukiwa kama mdau wa soka nchini, unazungumziaje suala hilo? Je, ni sahihi kuelekeza lawama kwa Amunike kwa kutomuita Ajib kwenye kikosi cha Stars? Tuma maoni yako ukianzia na jina lako kamili na mahali ulipo kwenda namba 0718540757.

Wiki iliyopita kulikuwa na mada inayozungumzia juu ya maoni ya wadau mbalimbali wa soka nchini kuhusu mechi ya Watani wa Jadi, wa Simba na Yanga.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Septemba 30 mwaka huu, ulimalizika kwa mahasimu hao kutoka sare ya bila kufungana.

Licha ya matarajio ya wengi pengine upande mmoja ungeibuka na ushindi na kutoka kifua mbele, mambo yalikuwa tofauti.

Wachangiaji wengi walituma maoni yao huku kila mmoja akitoa tathmini yake juu ya alivyoutazama mchezo huo kwa ujumla. Naitwa Sultan Athuman wa

Magomeni, Dar, mechi ilikuwa nzuri kwa upande wa Simba, walitawala vipindi vyote viwili, lakini kwa upande wa Yanga beki pamoja na kipa walifanya kazi zao vizuri. Naitwa Mudy wa

Kijitonyama Dar, kusema ukweli si vibaya wala si dhambi mimi kama wadau wengine tunazipongeza Yanga na Simba kwa kuhamasisha soka letu kimataifa kwa ushindani, ingawa ile sare imewanufaisha Yanga. Naitwa Samsom Christopher wa Ugweno,

mchezo huo ulikuwa mgumu, hasa kwa Yanga, kwani walielemewa sana na kushambuliwa, lakini nawapongeza kwa mbinu zao kupitia Kocha Zahera, lakini kwa Simba washambuliaji walishindwa kutumia nafasi. Naitwa Neema wa Mbezi, mimi kwa mtazamo wangu hatujaona ushindani ambao tulitegemea kulingana na uwezo wa timu zote mbili, maana mechi ilichezwa na upande mmoja ambao ni Simba, ingawa hawakupata ushindi.

Naitwa Nickson Mbogella wa

Tunduma, Simba walikuwa vizuri kila idara, isipokuwa kocha aongeze mbinu za ufungaji mabao, kwani wana wachezaji wa kulipwa wengi na wazuri. Naitwa Sele Njende wa

Mbagala, tathmini yangu ni kwamba, mpira wa Simba na Yanga ni kwamba Simba walikuwa na presha na ule mchezo hawakuwa makini, tofauti na Yanga, ambao waliweza kutumia mbinu za mwalimu, japo kuna baadhi ya wachezaji walimwangusha.

Naitwa Babu Beku wa Mwandege,

Mkuranga, Yanga ilifeli kwa mbinu zote katika mechi ile, maana mipira mingi ilipita kwa mabeki wake, lakini kazi kubwa aliifanya kipa. Kwa jina naitwa Blayson Maganjila wa

Dar, mchezo ulikuwa mkali kwa kila timu, ila kilinikera kitendo cha Ajib kupiga mpira nje.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.