ROONEY ATAKA VYOMBO VYA HABARI VIACHANE NA MOURINHO, AITETEA MAN U MWACHENI

Dimba - - Burudani Za Wasanii - WASHINGTON, MAREKANI

STRAIKA wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, anashangazwa na vyombo vya habari vinavyopoteza muda kutoa habari za Jose Mourinho na timu yake ya zamani. Mourinho na Manchester United imekuwa habari ya mjini katika vyombo vya habari kutokana na kile kinachoendelea ndani ya klabu hiyo kubwa nchini England. Lakini Rooney anaonyesha hafurahishwi na hali hiyo, huku akitupia lawama kwa vyombo vya habari ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikiripoti taarifa za timu hiyo na mwenendo wake. Jumamosi iliyopita, Manchester United walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United, baada ya kutanguliwa kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza. Ushindi huo umekuja kwa Manchester United baada ya michezo minne kupita bila kupata ushindi wowote na kuzua hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo na kibarua cha Mourinho. “Sipendezwi na vyombo vya habari vinavyoripoti kuhusu Manchester United, wanachocheza zaidi kuliko uhalisia ambao upo ndani ya klabu hiyo,” alisema Rooney. Hivi sasa Rooney anakipiga katika klabu ya DC United ya Marekani ambayo alijiunga akitokea Everton, mpaka sasa kafunga mabao sita kwenye michezo 11 aliyocheza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.