Stars yapaa kibabe kuifuata Cape Verde

Dimba - - News - NA TIMA SIKILO

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimeondoka kibabe jana usiku kuelekea nchini Cape Verde kukipiga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), unaotarajiwa kupigwa keshokutwa nchini humo.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, amesema kikosi chake kipo tayari kwa shoo hiyo ya kibabe, ili kuendeleza matumaini ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon. Alisema wanakwenda kukipiga na timu nzuri, lakini wamefanya maandalizi ya kutosha na yote hayo yatakwenda kuonekana uwanjani siku ya mchezo huo.

Amunike alisema, kazi wanayowaachia Watanzania ni kuwaombea dua warudi na pointi tatu muhimu ili kuchonga barabara ya kuelekea Cameroon kilaini.

ìKikosi kimefanya maandalizi ya kutosha, tunashukuru viongozi, wadhamini na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano ambao wameonyesha, kikubwa tunaomba Watanzania waendelee kuiombea timu iweze kurudi nyumbani na pointi tatu,î alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.