Simba waipiga bao Yanga kimataifa

Dimba - - News - NA MAREGES NYAMAKA

UNAKUMBUKA lile neno la Yanga kuwa wao ni wa kimataifa lililonogeshwa na msemaji wao wa zamani, Jerry Muro, lakini sasa ni kama mambo yamewageukia kwa namna taswira ilivyo upande wa Simba.

Ukimataifa huo si wa kupanda ndege kwenda kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho wala Ligi ya Mabingwa Afrika, isipokuwa ni kwamba Simba imekuwa ya kipekee wachezaji wake wengi kuitwa kucheza timu za mataifa yao.

Wekundu hao wa Msimbazi wametoa jumla ya wachezaji watano, tofauti na ilivyo kwa watani wao wa jadi, Yanga, ambao hawajatoa mchezaji hata mmoja, isipokuwa wazawa pekee ndani ya Taifa Stars.

Nyota hao ni Jjuuko Murshid, Emmanuel Okwi(Uganda), Haruna Niyonzima, Middie Kagere wote wa Rwanda na Clatous Chama kwenda kuitumikia Zambia, huku kwa upande wa Azam akiwa mmoja pekee, Tafadzwa Kutinyu (Zimbabwe).

Wakali hao wote watakuwa na kazi moja tu wikiendi hii, kupambana kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika(Afcon) 2019 Cameroon.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.